Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewasihi wanafunzi wanao soma katika Taasisi yetu ya Elimu ya Kolowa Technical Training Institute (KOTETI) kuwa waadilifu katika kazi pindi watakapomaliza mafunzo yao ya ufamasia katika ngazi ya Stashahada na Astashahada, ameyasema hayo leo tarehe 6/2/2023 katika ziara yake ya kikazi katika taasisi yetu ambayo  inamilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki .

Askofu Dkt. Mbilu ameupongeza uongozi  pamoja na watumishi kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa elimu bora na yenye kiwango kikubwa ambayo imedhihirishwa na uwepo wa maabara ya kisasa,mazingira salama na yenye utulivu.

[su_custom_gallery source=”media: 2228″ limit=”35″ width=”770″ height=”520″]

Nae Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya KOTETI  mfamasia Mbowela Kibelenge ameushukuru uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu kwa ushirikiano wanaouonyesha na kuahidi kufanya mambo makubwa yatakayoleta mabadiliko makubwa hususani kuhakikisha Taasisi hiyo inafikia ngazi ya Chuo Kikuu.

[su_custom_gallery source=”media: 2229″ limit=”35″ width=”770″ height=”520″]