MKUU WA CHUO CHA KOLOWA TECHNICAL TRAINING INSTITUTE (KOTETI) KILICHOPO KATIKA MAJENGO YA KILICHOKUWA CHUO KIKUU CHA SEBASTIAN KOLOWA MEMORIAL UNIVERSITY  (SEKOMU) MAGAMBA LUSHOTO TANGA.
 Anawatangazia udahili wa mafunzo kada ya sheria.
Astashahada (Certificate in Law) na Stashahada (Diploma in Law) kwa mkupuo wa mwezi wa tatu (March intake)
A. SIFA ZA KUJIUNGA NI KAMA IFUATAVYO
I. ASTASHAHADA (CERTIFICATE IN LAW)
 Muombaji awe na ufaulu wa angalau alama D nne (4) katika masomo yasiyo ya dini na somo la kiingereza ni lazima.
II. STASHAHADA (DIPLOMA IN LAW)
 Muombaji awe na ufaulu wa angalau principal pass 1 na subsidiary moja za kidato cha sita AU
 Astashahada ya sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na NACTVET
B. NAMNA YA KUJIUNGA
 Fomu za kujiunga zinapatikana chuoni (KOTETI), kwenye tovuti ya Chuo (www.koteti.ac.tz) na Ofisi za KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.Fomu  zijazwe na kutumwa chuoni au kwa barua pepe ya admin@koteti.ac.tz kabla ya tarehe 28/02/2025.
 Ada ni Tsh. 965,000/= na italipwa kwa awamu
 Hosteli nzuri na huduma ya chakula vinapatikana kwa bei nafuu kabisa ndani ya Chuo.
Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0716393887 au 0747067564 au 0712811420.
Wote mnakaribishwa