TAARIFA KWA UMMA KUHUSU USAJILI KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA PROGRAMU ZA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI KWA MWAKA WA MASOMO 2022/2023

Baraza laTaifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linapenda kuujulisha umma kwamba zoezi la uchaguzi kwa wanafunzi walioomba kujiunga na programu za Afya na Sayansi Shirikishi kwa mwaka wa masomo 2022/2023 lilikamilika rasmi tarehe 30.09.2022. Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na programu hizo walitakiwa kuripoti vyuoni kuanzia tarehe 3 hadi 18 Oktoba, 2022 na masomo yalianza rasmi tarehe 17 Oktoba, 2022.

Hivyo, vyuo vinaelekezwa kuwasajili wanafunzi waliofika vyuoni mpaka tarehe 31 Oktoba, 2022. Waombaji wote waliothibitisha kutojiunga na Chuo husika waondolewe kwenye mfumo.

Baraza linatoa tahadhari kwa vyuo kutowapokea waombaji ambao hawakuomba nafasi za masomo kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System – CAS). Pia, waombaji ambao hawakufanya hivyo wasipokelewe kwakuwa hawatatambulika kama wanafunzi halali. Aidha, Baraza litachukua hatua kali kwa vyuo vitakavyobainika kupokea wanafunzi ambao hawakudahiliwa kupitia CAS.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (NACTVET)

21/10/2022